Alhamisi, 22 Oktoba 2015

TATIZO LA VIFO KWA SAMAKI AINA YA KAMBALE

African-catfish-fingerlings1


Kwa wale ambao tuemefuga samaki aina ya kambale kwenye mabwawa ni wazi jambo hili tumekutana nalo. Na hata kama hujakutana nalo ni vyema ukapata hii elimu ili tatizo likianza ujue wapi kwa kuanzia.
Kwa maelezo zaidi pitia link hii hapa chini;

http://farmerscreed.com/how-to-reduce-fingerling-mortalities-on-your-fish-farm




Jumatatu, 19 Oktoba 2015

UZALISHAJI WA VIFARANGA VYA SAMAKI KIBIASHARA














Hii ilikuwa ni ziara ya kumtembelea mdau wa ufugaji wa samaki EDEN AGRI AQUA FARMING LTD, ambaye amejikita katika kuzalisha vifatanga vya samaki aina ya Sato na Kambale.
Yupo Dar-es-salaam maeneo ya Pugu Kinyamwezi.

Kama unahitaji vifaranga vya samaki wanapatikana kwao.

Je na wewe unahitaji kujiunga na fani hii?

Wasiliana nasi kwa 0655637026 kwa maelezo zaidi.

Jumatano, 7 Oktoba 2015

GHARAMA ZA KUPATA HUDUMA ZETU

Habari ya Leo Ndugu wadau na wasomaji. Baada ya kuwasiliana na baadhi ya watu ambao wamepata hamasa ya ufugaji wa samaki, nimegundua wengi wao wamekuwa wakisita kututafuta kwa kikwazo kikubwa ni kushindwa kufahamu gharama ambazo zitahusika ili waweze kupata huduma hii.

Gharama zetu siyo kubwa, na napenda kuchukua nafasi hii kuziweka ubaoni aina ya huduma ambazo zinaweza kupatikana ili ifahamike kwa kila mmoja wenu.

Huduma hizo ni kama ifuatavyo:-

  1. Kukagua eneo kama linafaa kwa ufugaji wa samaki na kutoa ushauri kwa siku. 
  2. Kusimamia uchimbaji na utengenezaji wa bwawa la samaki kwa siku.
  3. Kutengeneza chakula bora cha samaki kwa siku.
  4. Kuelekeza namna ya kuzalisha samaki(Kambale/Tilapia) kwa siku.
  5. Kwenda kukutafutia mbegu bora za samaki kwa siku.
  6. Kutoa USHAURI/MAFUNZO kwa kikundi cha watu, au mtu mmoja kwa siku.
Malipo ya huduma hizo hapo juu ni Tsh.100,000/= kwa siku 1 Tu.

Gharama hii ni nje ya nauli ya mtaalamu kufika huko uliko au unakotaka kuweka mradi wa kufuga samaki.

Vilevile, kwa wale ambao tayari wamesha anza ufugaji wa samaki katika mabwawa, lakini hawana zana bora za kuvulia samaki yaani NYAVU, mkihitaji kutengenezewa nyavu kwa ajili ya mabwawa ya kawaida inawezekana. Gharama yake itategemea na ukubwa wa mabwawa husika.

Kwa hayo machache, nawakaribisha nyote.
Ahsanteni.