Jumatano, 7 Oktoba 2015

GHARAMA ZA KUPATA HUDUMA ZETU

Habari ya Leo Ndugu wadau na wasomaji. Baada ya kuwasiliana na baadhi ya watu ambao wamepata hamasa ya ufugaji wa samaki, nimegundua wengi wao wamekuwa wakisita kututafuta kwa kikwazo kikubwa ni kushindwa kufahamu gharama ambazo zitahusika ili waweze kupata huduma hii.

Gharama zetu siyo kubwa, na napenda kuchukua nafasi hii kuziweka ubaoni aina ya huduma ambazo zinaweza kupatikana ili ifahamike kwa kila mmoja wenu.

Huduma hizo ni kama ifuatavyo:-

  1. Kukagua eneo kama linafaa kwa ufugaji wa samaki na kutoa ushauri kwa siku. 
  2. Kusimamia uchimbaji na utengenezaji wa bwawa la samaki kwa siku.
  3. Kutengeneza chakula bora cha samaki kwa siku.
  4. Kuelekeza namna ya kuzalisha samaki(Kambale/Tilapia) kwa siku.
  5. Kwenda kukutafutia mbegu bora za samaki kwa siku.
  6. Kutoa USHAURI/MAFUNZO kwa kikundi cha watu, au mtu mmoja kwa siku.
Malipo ya huduma hizo hapo juu ni Tsh.100,000/= kwa siku 1 Tu.

Gharama hii ni nje ya nauli ya mtaalamu kufika huko uliko au unakotaka kuweka mradi wa kufuga samaki.

Vilevile, kwa wale ambao tayari wamesha anza ufugaji wa samaki katika mabwawa, lakini hawana zana bora za kuvulia samaki yaani NYAVU, mkihitaji kutengenezewa nyavu kwa ajili ya mabwawa ya kawaida inawezekana. Gharama yake itategemea na ukubwa wa mabwawa husika.

Kwa hayo machache, nawakaribisha nyote.
Ahsanteni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni