Jumatano, 15 Februari 2017

"BIOSECURITY" ina umuhimu gani kwenye shamba lako?

Click link hii ili Uifunze hapa umuhimu wa usalama wa mazingira ya kufugia samaki (Biosecurity).
 


Kutokana na kuongezeka kwa Magonjwa ya Samaki katika nchi zinazotuzunguka zikiwemo Congo, Zambia, Msumbiji, Namibia, Angola na Afrika ya kusini,  kuna umuhimu wa kuweka Mikakati ya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa yasiyo na Mipaka kaingia na kuleta madhara. Maelezo haya yametolewa na Dr. Hamis Nikuli Mtaalamu wa Afya na tiba kwa Viumbe wanaofugwa kutoka Idara ya Ukuzaji viumbe Kwenye Maji-Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.


Jumatatu, 13 Februari 2017

SEMINA JUU YA USALAMA WA MAZINGIRA YA KUFUGIA SAMAKI NA MAGONJWA YA SAMAKI
Pichani chini ni Washiriki wa Semina ya Usalama wa Mazingira ya Kufugia Samaki na Magonjwa, Zaidi ya Mameneja kumi kutoka mashamba mbalimbali ya samaki likiwemo shamba la EDEN AGRI-AQUA CO.LTD walishiriki.

Kaimu Katibu Mkuu sekta ya Uvuvi Dr. Erasto Mosha alifungua Semina hiyo na kuwaasa washiriki kuzingatia kitakachofundishwa kwakuwa Ufugaji wa Samaki ni biashara inayolipa hapa nchini.

 

Alhamisi, 2 Februari 2017

SEMINA YA UFUGAJI SAMAKI KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINIMnamo tarehe 27/01/2017 kampuni ya ROFACOL CO. LTD inayojihusisha na masuala ya ufugaji samaki Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini yenye ofisi zake Kyela Mjini iliandaa semina juu ya Ufugaji Samaki. Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kyela, ndiye alikuwa mgeni rasmi na Mfunguzi wa semina hiyo.

Katika semina hiyo watu 130 walihudhuria kutoka katika Mikoa yote iliyoko Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini na kulikuwa na watoa mada wanne (4) ambao waliwakilisha taasisi zao, kutoka ROFACOL CO.LTD, WIZARA YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI, TAFIRI, OFISI YA MKUU WA WILAYA KYELA. Vilevile walikuwepo wawakilishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mbeya,Ofisi ya Uhamiaji, na Afisa Mtendaji Kyela.

Dhumuni.
1. Dhumuni kubwa la semina hiyo lilikuwa kutoa elimu juu ya ufugaji samaki kwenye mabwawa na vizimba,
2. Kuhamasisha na kutoa elimu juu ya sera za ukuzaji viumbe kwenye maji
3. Kutoa elimu juu ya aina ya samaki wanaofaa kufugwa katika maeneo wanayopatikana.

Maazimio.

Maazimio sita yaliyofikiwa katika semina hiyo kama ifuatavyo:- 


 1. Taratibu zote za uanzishwaji wa shughuli za ufugaji samaki na utengenezaji wa chakula cha samaki kibiashara zifuatwe, kulingana na Sera na Kanuni za Uvuvi zinavyo elekeza. 
 2. Serikali imeshauriwa kuweka kipaumbele cha kuongeza idadi ya wataalam wa ufugaji wa samaki hasa katika ngazi za chini ili wawe karibu na wafugaji wa samaki. 
 3. Taarifa ya takwimu za mabwawa na vizimba ukanda wa nyanda za juu kusini zitolewe kwenye mamlaka husika ili kuwezesha upatikanaji wake zinapohitajika. 
 4.  Uwekaji na utunzaji wa kumbukumbu kwa kila mfugaji wa samaki ulitajwa kama changamoto katika maendeleo ya ufugaji wa samaki. 
 5. Kwa kuzingatia umuhimu uliyo onekana katika semina hiyo, maazimio yalitolewa kwamba kila baada ya miezi mitatu (3) semina kama hiyo ifanyike katika kanda nyingine.


 
 


Ijumaa, 8 Aprili 2016

UNAWEZAJE KUTENGENEZA BWAWA LA KUFUGIA SAMAKI?


Zipo namna mbalimbali za utengenezaji wa bwawa la samaki, kulingana na aina ya bwawa lenyewe.
Aina ya bwawa la kufugia samaki.
 • Bwawa la kuchimba udongo bila kujengea "Earthen Pond" ambalo litakuwepo mahali ambapo udongo unaruhusu kutuwamisha maji. Mara nyingi kuta zake hushindiliwa na kupandwa nyasi ili kupunguza nguvu ya maji kasababisha mmomonyoko wa udongo. 


 • Bwawa la kuchimba udongo bila kujengea "Earthen Pond" ambalo litakuwepo mahali ambapo udongo hauruhusu kutuwamisha maji, litatandikwa Karatasi la "Nylon"/"Polythene sheet" ili kuzuia maji yasipotee ardhini. 
 •  

 • Bwawa la kuchimba udongo na kujengea kwa Matofali, Cementi na Zege;
 • Kwenda chini ya ardhi "Earthern concrete pond"
 • Kwenda juu ya ardhi "Raised Conrete Pond" 

Je, unalo eneo linalofaa kwa ajili ya ufugaji wa samaki? Wasiliana nasi kwa namba 0655637026 , Upate Msaada na Ushauri wa Kitaalam.

SAMAKI KAMBALE WA KUFUGWA WANAUZWA

Habari ya leo wapendwa wasomaji wa Blog ya UFUGAJI BORA WA SAMAKI.
Ni matumaini yangu hamjambo na kazi ya ujenzi wa taifa la Tanzania inaendelea vyema.
Mbali na hilo, Yupo Mdau Mwenzetu, aliye pandikiza samaki aina ya Kambale na kuwafuga mpaka wamefikia hatua ya kuvunwa, waende sokoni.
Samaki hao wana wastani wa 1.5kg mpaka 2.0 Kg. Anauza kila 1Kg kwa Tsh.8000/=.
Hivyo basi nawashirikisha nanyi kumuunga Mkono ili ayaone matunda ya kazi aliyo ifanya, katika uzalishaji wa chakula bora na ujenzi wa Taifa lake. Yupo Kimara Korogwe karibu na kanisa la KKKT Kimara, Mawasiliano yake ni 0754426256, au Nipigie 0655637026 kwa Maelekezo Zaidi.
KARIBUNI

Alhamisi, 21 Januari 2016

Uchimbaji wa Mabwawa ya ufugaji wa samaki kibiashara

Ndugu Mdau wa Ukurasa huu, ninayo furaha kukushirikisha kuitizama Video hii ujionee jinsi ambavyo wadau wengine wamehamasika katika tasnia hii ya ufugaji samaki kibiashara. Video hiyo utaipata kwa link ifuatayo Uchimbaji wa Mabwawa ya Kufugia Samaki Kibiashara

Image result for ufugaji wa samaki kibiashara+uganda

Ijumaa, 15 Januari 2016

FURSA KUTOKANA NA MAZAO YA UVUVI

Wadau nimeona ni vyema nikawashirikisha nanyi kuitazama na kuwasikiliza watoa mada katika video inayopatikana kwenye link ifuatayo;

Uchakataji wa mazao ya Uvuvi 

Dagaa wanao kaushwa kwa njia ya Jua katika Vichanja

Dagaa waliokaangwa kwa mafuta na Kuhifadhiwa katika vifaa Maalumu

Dagaa waliokauka kwa njia ya Jua