Jumamosi, 29 Juni 2013

UFUGAJI WA PEREGE

Ufugaji wa samaki
Ufugaji samaki ni kazi ya kupanda, kukuza na kutunza samaki katika mabwawa au uzio (uliotengenezwa kwa vyuma, nyavu 
au miti) au eneo lolote ambalo udhibiti wake yako chini ya mamlaka ya mfugaji mwenyewe. Mabwawa yaweza kuwa ni ya 
kuchimbwa na watu (japokuwa ya asili pia huweza kutumika) wakati uzo inaweza ikawa imewekwa katika eneo lolote 
lililo na maji kama ziwa na hata bahari.
Ufugaji samaki kwa kiasi fulani si sawa na ukuaji samaki katika mito, maziwa na bahari. Tofauti iko katika huduma inayotolewa kwa samaki wafugwao na idadi ya samaki wanaopaswa kuwamo ndani ya eneo husika. Samaki waliofugwa huhitaji kulishwa na kuhudumiwa.
Ufugaji wa samaki si kitu kipya kabisa hapa Tanzania. Baadhi ya Watanzania wamekuwa wakifuga samaki katika mabwawa 
hata kabla ya nchi yetu kupata uhuru. Lakini baadhi ya wafugaji wamekuwa wakitoa matunzo hafifu kiasi cha kufanya 
mavuno kutokuwa mazuri. Kwa miaka ya karibuni, serikali imetilia mkazo utoaji elimu (ugani) wa ufugaji samaki ili 
kuboresha mafanikio yake. Kuchapishwa kwa kitabu hiki kitasaidia kuongeza uelewa wa wakulima wafugaji wa 
samaki katika shughuli nzima ya ufugaji samaki nchini.

Faida za ufugaji samaki
Ufugaji samaki una faida nyingi sana, baadhi ni haya:
1.  Chakula bora chenye uto-mwili (protini) muhimu inayohitajika kujenga mwili.
2.  Kujipatia kipato baada ya kuuza samaki waliofugwa.
3.  Kuboresha kazi nyingine za kilimo kama bustani ya mboga, ufugaji wa ng’ombe, bata, kuku, nguruwe, bustani ya miti, n.k.
4.  Huwezesha kutumia rasilimali ambayo isingekuwa ikitumika kama kusingekuwa na ufugaji samaki kama vile eneo 
     la ardhi lenye maji maji, pumba za mahindi na mpunga, na mabaki ya mboga mboga kutoka bustanini kwa kulishia samaki.
5.  Eneo la bwawa huwa ni sehemu nzuri ya mapumziko.
  
Hatua muhimu katika shughuli za ufugaji samaki
1.     Uchaguzi wa mahala panapofaa kwa ajili ya kuchimba bwawa la samaki.
2.     Tathmini ya umbo na ukubwa wa bwawa
3.     Uchimbaji wa bwawa.
4.     Uingizaji na utoaji wa maji katika bwawa.
5.     Uwekaji wa mbolea na (majivu).
6.     Upandaji wa vifaranga vya samaki.
7.     Ulishaji wa samaki na matunzo mengine bwawani.
8.     Uvunaji wa samaki na aina ya nyavu/zana zifaazo kutumika.
9.     Uhifadhi wa mbegu kwa ajili ya mzungoko mwingine wa upandaji samaki bwawani.

Vigezo muhimu katika kuboresha uzalishaji 
Joto au ubaridi wa maji katika sehemu husika huweza kuongeza au kupunguza hamu ya ulaji wa samaki na hivyo ukuaji wake. 
 • Chakula cha samaki (cha asili na cha ziada), aina ya chakula na kiasi kinachopatikana.
 • Uwingi wa samaki waliomo bwawani kulinganisha na ukubwa wa bwawa.
 • Ubora wa vifaranga (quality) waliopandwa. Vifaranga wenye ubora mruzi huwa na uwezo wa kukua haraka.
 • Muda uliotumika kuzalisha samaki. Japokuwa samaki hukua haraka, wanahitaji muda wa kutosha kufikia ukubwa unaofaa kwa mahitaji ya mkulima au wa soko. 
 • Uwepo wa magugu na mimea isiyohitajika bwawani.
 • Uwepo wa maadui wa samaki (predators).
 • Kuwa na tabia ya kuvua bwawa kila baada ya miezi 6 hadi 9 kwa kulikausha ili kuboresha mazingira yake.
 • Huduma inayotolewa bwawani husaidia  kupatikana samaki wakubwa na wenye afya.Maoni 4 :

 1. hakika nimefurahi sana kupata maelekezo ya namna ya kufuga samaki. nahitaji kuchimba kisima lakini maelekezo ya namna ya kuchimba kisima hayajitosherezi kwa mfano:- kisima kinajengwa na tofari baadae unakandika na udogo mfinyanzi au inakuaje, nisaidie nielewe nahitaji kuchimba leo hata kesho

  JibuFuta
  Majibu
  1. Huwa tunaita Bwawa la kufugia samaki. Matofali na sementi vinaweza kutumika endapo udongo wa eneo unaloweka hilo bwawa una asilimia kubwa ya Mchanga, ambao hupoteza maji kwa wingi.

   Futa
 2. nina eneo la kutosha nahitaji msaada wa namna ya kuchimba kisima kwa ajili ya kufuga samaki aina ya perege kama nilivyosoma katika tovuti hii. naishi dar es salaam nitafarijika sana nikifunzwa namna ya kuchimba kisima kwa urefu na mapana

  JibuFuta
  Majibu
  1. Bwawa huwa linatakiwa kuwa na urefu wa wastani kati ya Mita 1.5 mpaka 1.8, upana na urefu unategemea eneo husika lina ukubwa gani...!

   Futa