Alhamisi, 11 Juni 2015

Ufugaji Mseto wa Sato na KambalePolyculture ni uzalishaji wa samaki aina mbili au zaidi ndani ya mazingira ya maji. Kwa kawaida polyculture hutokea katika mabwawa. Samaki aina ya kambare na sato wanaweza kutumika. Aina hizi za samaki zinafaa na huleta mafanikio mazuri.
Aidha vigezo vya kuchagua samaki kwa ajili  ya polyculture ni hivi hapa chini;

  • Kiwango cha juu ukuaji wa aina ya samaki;
  • Samaki wanaohitajika kwa wingi katika masoko;
  • Chagua aina wale ambayo wana kiwango cha juu cha ukuaji na kiwango cha chini cha vifo katika ukuaji;
  • Aina ambayo hawakupatwi na magonjwa kwa urahisi.samaki ambao ni phytoplankton vorous au omnivorous.

Katika  polyculture, masuala ya kuzingatia ni kama vile Chakula, Mavuno na Masoko yanahitajika kwanza.

Msongamano wa samaki katika bwawa  unaosababishwa na uzalianaji wa Sato (Oreochromis niloticus) ambao husababisha  mashindano katika kula chakula na matokeo yake ni mavuno ya samaki kuwa wadogo sana na thamani yao kushuka chini katika masoko. 

Moja ya mikakati ya kudhibiti kuzaliana kwa wingi kwa sato katika bwawa ni polyculture

Miaka michache iliyopita ,Kambare (Clarias gariepinus), wamechunguzwa na kujulikana kama wana uwezo mkubwa katika polyculture. 

Hata hivyo, idadi ya Sato inaweza kupunguzwa kwa ufugaji mseto wa Sato pamoja na samaki Predator. 


Fungua link hii hapa kupata maarifa zaidi.

http://www.ehow.com/about_5436585_polyculture-fish-farming.html
Huduma za ugani kwa  mkulima zinapatikana . Kwa yeyote aliyevutiwa na ufugaji huu wa samaki awasiliane nasi kwa namba 0655637026Hakuna maoni:

Chapisha Maoni