Alhamisi, 2 Februari 2017

SEMINA YA UFUGAJI SAMAKI KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI



Mnamo tarehe 27/01/2017 kampuni ya ROFACOL CO. LTD inayojihusisha na masuala ya ufugaji samaki Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini yenye ofisi zake Kyela Mjini iliandaa semina juu ya Ufugaji Samaki. Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kyela, ndiye alikuwa mgeni rasmi na Mfunguzi wa semina hiyo.

Katika semina hiyo watu 130 walihudhuria kutoka katika Mikoa yote iliyoko Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini na kulikuwa na watoa mada wanne (4) ambao waliwakilisha taasisi zao, kutoka ROFACOL CO.LTD, WIZARA YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI, TAFIRI, OFISI YA MKUU WA WILAYA KYELA. Vilevile walikuwepo wawakilishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mbeya,Ofisi ya Uhamiaji, na Afisa Mtendaji Kyela.

Dhumuni.
1. Dhumuni kubwa la semina hiyo lilikuwa kutoa elimu juu ya ufugaji samaki kwenye mabwawa na vizimba,
2. Kuhamasisha na kutoa elimu juu ya sera za ukuzaji viumbe kwenye maji
3. Kutoa elimu juu ya aina ya samaki wanaofaa kufugwa katika maeneo wanayopatikana.

Maazimio.

Maazimio sita yaliyofikiwa katika semina hiyo kama ifuatavyo:- 


  1. Taratibu zote za uanzishwaji wa shughuli za ufugaji samaki na utengenezaji wa chakula cha samaki kibiashara zifuatwe, kulingana na Sera na Kanuni za Uvuvi zinavyo elekeza. 
  2. Serikali imeshauriwa kuweka kipaumbele cha kuongeza idadi ya wataalam wa ufugaji wa samaki hasa katika ngazi za chini ili wawe karibu na wafugaji wa samaki. 
  3. Taarifa ya takwimu za mabwawa na vizimba ukanda wa nyanda za juu kusini zitolewe kwenye mamlaka husika ili kuwezesha upatikanaji wake zinapohitajika. 
  4.  Uwekaji na utunzaji wa kumbukumbu kwa kila mfugaji wa samaki ulitajwa kama changamoto katika maendeleo ya ufugaji wa samaki. 
  5. Kwa kuzingatia umuhimu uliyo onekana katika semina hiyo, maazimio yalitolewa kwamba kila baada ya miezi mitatu (3) semina kama hiyo ifanyike katika kanda nyingine.


 
 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni