Habari za Kazi Wasomaji wa Ukurasa huu.
Kwa ufupi ufugaji huu wa Samaki Kwanjia ya Vizimba ni teknolojia inayotumia Maji Machache, kuzalisha Samaki Wengi katika Eneo dogo lililo zungukwa na Nyavu Ndani ya Maji. Fungua link ifuatayo hapa chini kupata kujua mengi zaidi na kuruhusiwa kwa Ufugaji wa Samaki kwa njia ya Vizimba Tanzania. Ufugaji wa Samaki Kwa Njia ya Vizimba-Tanzania
Hivyo, Ili kuweza kupata Kibali cha kufanya Ufugaji wa Samaki kwa Njia ya Vizimba kama yalivyoandaliwa na Idara ya Ukuzaji wa Viumbe kwenye Maji-Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Ni wakati Mwingine tena tunakutana na kushirikishana katika masuala ya Uzalishaji wa Samaki na Mazao yake. Baada ya Kuona Ongezeko la Maombi ya Uanzishwaji wa Ufugaji wa Samaki kwenye Vizimba, nimeona ni vyema nikawaletea andiko hili kama Kichwa cha habari hapo juu kinavyo someka. Hii imechangiwa na baadhi ya Wawekezaji hasa wa ndani kutokuwa na uelewa wa kutosha jinsi au hatua za kufuata ili waweze kuwekeza katika Tasnia ya Ukuzaji Viumbe Kwenye Maji kwa njia ya Vizimba.
Kwa ufupi ufugaji huu wa Samaki Kwanjia ya Vizimba ni teknolojia inayotumia Maji Machache, kuzalisha Samaki Wengi katika Eneo dogo lililo zungukwa na Nyavu Ndani ya Maji. Fungua link ifuatayo hapa chini kupata kujua mengi zaidi na kuruhusiwa kwa Ufugaji wa Samaki kwa njia ya Vizimba Tanzania. Ufugaji wa Samaki Kwa Njia ya Vizimba-Tanzania
Hivyo, Ili kuweza kupata Kibali cha kufanya Ufugaji wa Samaki kwa Njia ya Vizimba kama yalivyoandaliwa na Idara ya Ukuzaji wa Viumbe kwenye Maji-Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Zifuatazo ni hatua
zinazopendekezwa kufyatwa ili mwekezaji aweze kupata kibali cha ufugaji samaki
kwenye vizimba.
- Mwekezaji au Mkulima ataanza kwa kutembelea mamlaka za uvuvi zilizopo kwenye eneo ambalo ufugaji kwa njia ya vizimba unatarajiwa kuwekezwa ili kupata taarifa ya mahitaji na matarajio ya uwekezaji,
- Katika hatua hii, mkulima au mwekezaji anatakiwa kuthibitisha uraia wake, kwa kuwasilisha vitambulisho au nyaraka zitakazothibitisha uraia wake,
- Kwa nyongeza, raia wa kigeni wanatakiwa kuwasilisha leseni ya uwekezaji zinazotolewa na mamlaka ya uwekezaji,
- Taarifa ya Ufanisi wa Eneo inayotolewa na Mamlaka husika kutoka eneo la Uwekezaji
- Mwekezaji au Mkulima anayetaka kuanzisha Ufugaji wa samaki kwenye Vizimba atatakiwa kuwasilisha katika Mamlaka husika kwa ajili ya kupitishwa, Mpango wa uanzishwaji ikiwa ni pamoja na Maelezo ya Makadirio na uendeshaji wa shamba kulingana na yaliyotajwa kwenye Mwongozo wa Ufugaji Samaki kwenye Vizimba pamoja na habari zifuatazo; Majina ya Mameneja na Anwani za Taasisi na, aina ya teknolojia ya Ukuzaji Viumbe kwenye Maji itakayo tumiwa,
- Mpango wa kudhibiti majitaka ikiwa ni pamoja na hatua za matibabu ya majitaka ya shamba katika mazingira na hatua za uchunguzi ili kuepuka kutoroka kwa samaki wanaofugwa,
- Kibali cha Matumizi ya Maji endapo matumizi yatazidi 400m3 kwa siku,
- Ushahidi wa kushirikishwa jamii na mashirikiano ya kijamii jirani na eneo la uwekezaji
- Hati ya Usajili wa biashara “Certificate of incorporation” and “Registration of business
- Leseni ya Biashara,
- Ushahidi wa Chakula cha Samaki kinapopatikana kutoka kwa chanzo kilichothibitishwa,
- Ushahidi wa Vifaranga vya Samaki vinapopatikana kutoka kwa chanzo kilichothibitishwa,
Ikiwa mahitaji haya yatatimizwa,
mwekezaji/mkulima atapewa kibali cha muda wa miaka miwili ya kuanzisha na
kufanya shughuli ya ufugaji samaki kwenye Vizimba. Katika hatua hii, Mkulima/Mwekezaji
anaweza kuanzisha shamba la samaki kwenye eneo lililokubaliwa. Waombaji
wanaoidhinishwa wanapewa idhini na vyeti, na huongezwa kwenye orodha ya vyeti
vya kuthibitishwa, kuzalisha na kuuza mazao ya ufugaji wa samaki katika soko la
ndani na / au nje ikiwa yanakidhi mahitaji ya Soko la kuuza Nje.
Maombi mapya yatafanyika mara kwa mara wakati
wowote kama mabadiliko makubwa yamefanywa kwa Mpango uliothibitishwa awali.
Wakati wa uendeshaji na uanzishwaji, wakulima au wawekezaji wanatarajiwa
kuzingatia Sera zote zinazohusiana na Kilimo cha Samaki.
Mamlaka husika ya Ufugaji wa Samaki itafuatilia
shughuli za kilimo cha Samaki kwa miaka miwili ya kwanza na ikiwa ni ya
kuridhisha, Kibali cha uendeshaji kwa muda mrefu kitatolewa.
Hata hivyo, leseni za uanzishwaji na uendeshaji wa Kilimo cha Samaki kwenye
Ziwa Victoria hazitatolewa kwa zaidi ya Miaka Kumi (10) Mfululizo.